MCHEPUKO SIO DILI!

Mke wangu alisajili line mpya jina la Jenifer Godson bila mimi kujua.
Jana usiku nimerudi home akaniomba elfu 10 akasuke.
Nikajibu sina elfu 10 nikampa buku 2
Wakati tumelala, Mara Paa msg katika simu yangu
"HI MY LOVE".
Kidume nikatoka nje nikaenda toilet, nikaijibu:
"we nani"
MSG: ni mimi Jane Msambwanda".
Kusikia Msambwanda, mshipa wa ubongo ukanicheza.
MIMI: Jane Msambwanda wa wapi tena?"
MSG: Bwana baby nawe,si pale unapokulaga kila siku?"
MIMI: "ooh,kumbe unaitwaga Jenifer, namba yangu umeipata wapi?
MSG: "nimepewa na rafiki yako DJ Tipwil, nakupenda sana handsome, sema huwa naogopaga kukwambia, ila mi sijiwez juu yako, yaani kila ukija kula, natamani usiondoke, nikwambie yaliyomo moyoni mwangu, nateseka sana mwenzio"
MIMI: Jamani pole mpenzi, hata mimi nilikuwa nakupenda, yaan kila nikiona huo msambwanda nahisi mzunguko wa damu kubadilika, I love you too honey.
MSG: Basi mpenzi ,nikuombe kitu
MIMI: aah,sema tu
MSG: naomba elfu 50
MIMI: nakutumia sasa ivi"
(NIKATUMA)
MSG: Waaoo asante mume wangu, haya rudi ndani tulale, mi mkeo MAMA KIDUKU hapa
πŸ™†‍♂πŸ™†‍♂πŸ™†‍♂
🎼_hapo ndo utaukumbuka wimbo wa dunia Lukumba lukumba🎼_


tunakukumbusha tembelea na vipengele vingine UJIFUNZE na kufurahi ukiwa nasi, hata siku moja usiache kupita kuna vipya tumekuandalia

Comments

Popular posts from this blog

MAHUSIANO KWENYE BONGO MOVIES 😁😁

UTANI KIDOGOπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€